Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 6 YA 31

Bwana Yesu ametumia mitego miwili ya maadui zake ili aweke bayana mafundisho mawili muhimu kwa vizazi vyote. Kwanza, ni wajibu wa kila raia wa nchi kulipa kodi halali za serikali. Ndivyo pia Paulo anavyoeleza katika Rum 13:1:Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Pili, mwanadamu anaweza kujenga uhusiano na Mungu wakati huu tu akiwa hai duniani. Jambo hili la kujenga uhusiano na Mungu, kama hujafanya, haliwezekani baada ya kifo. Twaitwa kuweka maisha yetu mikononi mwa Mungu leo, tukiwa bado tuko hai na wenye nguvu na akili timamu.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz