Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 24 YA 31

Zamani Mungu alisema nasi kwa njia ya manabii, na hakika walifanya kazi kubwa ya kueneza ujumbe wa Mungu. Kwa sasa Yesu amekuja kwetu, hivyo twaweza kuzungumza naye moja kwa moja. Yesu ameondoa kiambaza kilichotutenga na uwepo wa Mungu alipofanya utakaso wa dhambi.Akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu(m.3). Hivyo njia yetu kwa Mungu iko wazi. Yesu amekuja kutuletea wokovu. Uwepo wake kwetu ni mng’ao wa wokovu kwetu katika maisha yetu. Hii ni neema ya ajabu. Mwamini Yesu, nawe utapata wokovu na kuwa mrithi wa uzima wa milele.

Andiko

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz