Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 28 YA 31

Mafundisho haya hayahusu tu jamii ya watu, lakini pia kanisa. Hivyo yanahitaji kuzingatiwa sana na Wakristo na kipekee na viongozi wa kanisa!Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora kuliko wingi wa mali wa wasio haki(m.16). Ukijipatia mali kwa njia isiyo haki huna heri, na yale uliyo nayo hayakupi raha kama ulivyotegemea. Bali ukiridhika na hali aliyokupa Bwana na kuzidi kumwambia mahitaji yako, hutakosa baraka zake. Utaona raha kuliko asiye haki, ingawa ana mali nyingi. Zingatia zaburi inavyofafanua tofauti ya mwenye haki na asiye haki:Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu. ... [Mwenye haki] ajapojikwaa hataanguka chini, Bwana humshika mkono na kumtegemeza. Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa(m.21 na 24-26)!

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz