Zab 37:16-26
Zab 37:16-26 SUV
Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi. Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali BWANA huwategemeza wenye haki. BWANA anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele. Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba. Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka. Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu. Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi, Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa. Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza. Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.