Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 37:16-26

Zaburi 37:16-26 NEN

Bora kidogo walicho nacho wenye haki kuliko wingi wa mali wa waovu wengi; kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, lakini BWANA humtegemeza mwenye haki. BWANA anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele. Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. Lakini waovu wataangamia: Adui za BWANA watakuwa kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi. Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu. Wale wanaobarikiwa na BWANA watairithi nchi, bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali. Kama BWANA akipendezwa na njia ya mtu, yeye huimarisha hatua zake, ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana BWANA humtegemeza kwa mkono wake. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula. Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti. Watoto wao watabarikiwa.