Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Leo tumepewa kutafakari miisho ya watu wa aina mbili: mtu mnyofu na mtu mwovu. Mtu mnyofu hujiepusha na uovu na hutafuta kutenda mema. Kwa upande mwingine, mtu mwovu hutafuta kumwangamiza mtu mnyofu. Je, miisho yao ni nini?Umtazame mtu mnyofu, maana mwisho wake huyo mtu niamani. ... [Wakati]wasio haki mwisho waowataharibiwa.Sababu ya tofauti hiyo kubwa ni kwambawokovu wa wenye haki una Bwana(m.37-39). Kuifuata njia ya haki na kumngoja Bwana kuna faida ya kudumu katika maisha haya na hata milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz