Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano
Mkate huu aliotoa Yesu usiku wa Pasaka ni uhalisi wa fumbo la nyama ya kondoo wa Pasaka na mana ya jangwani. Kuhusu mwana-kondoo ambaye atakuwa hana ila, imeandikwa:Mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana(Kut 12:11).Na kuhusu mana imeandikwa kuwawana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arobaini, hata walipofikilia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikilia mipakani mwa nchi ya Kanaani(Kut 16:35). Pia ni maana halisi ya fundisho la Yesu katika Injili ya Yohana:Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe. ...Mimi ndimi chakula cha uzima(Yn 6:35 na 48). Divai waliyokunywa ni uhalisi wa fumbo la damu iliyowaokoa wana wa Israeli kule Misri:Nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri(Kut 12:12-13). Na sisi kila tulapo mkate na kunywa divai twakiri na kutangaza tumaini la wokovu wetu unaotokana na kazi ya Yesu Kristo kuutoa mwili na damu yake kwa ukombozi wa wanadamu wote.Kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo(1 Kor 11:26).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz