Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano
Sikukuu ya Pasaka ina maana ya wokovu wetu kwa kifo cha Yesu. Tafakari Musa anavyowaambia wazee wa Israeli katika Kut 12:21-23:Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.Yesu ndiye Mwana-kondoo wa Pasaka ya Wakristo. Leo tumesoma Yesu akijiandaa mbele ya wanafunzi wake kwenda kufa, awe kafara ya dhambi za watu wote. Na Yuda anadhihirisha uwezekano wa mtu kuwa Mkristo kwa miaka mingi, lakini moyoni mwake asimthamini Yesu. Tamaa ya fedha inaweza kumvuta mtu mpaka aasi mafundisho na maonyo ya Mungu, na kumfanya aukaneUkristo. Tuombe Mungu atupe uthabiti katika imani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz