Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Katika huduma ya Yesu tunasikia mara chache kwamba ugonjwa wa mtu ulisababishwa na pepo. Jana tulisoma kwamba alimponya mtu mwenye ugonjwa wa kawaida wala hakuwa na pepo. Lakini leo anamponya mtu ambaye anaonekana kuwa na ugonjwa wa kawaida, hata hivyo udhaifu wa mwili wake ulisababishwa na pepo. Hata Tanzania haya yanatokea. Lakini tusifikiri kwamba magonjwa yote husababishwa na pepo. Ni mara chache tu. Tusimtie hofu mtu kwa kudai kwamba ana pepo mchafu ikiwa ana ugonjwa wa kawaida tu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/