Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

SIKU 9 YA 31

Kupaa kwa Yesu ni tendo la Yesu kuondoka kimwili hapa duniani na kwenda mbinguni. Kuna faida pia kwetu, kwani Yesu aliahidi kwenda kutuandalia makao ambayo wote wanaomwamini wataishi naye baadaye. Pia alitoa ahadi ya kutuletea Roho Mtakatifu ili atuongoze, atutie nguvu na kutufariji katika huduma yetu:Mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi(Mdo 1:8). Mpaka leo Yesu yupo kati yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu, na baraka zake zipo kwa wote wanaoliitia jina lake. Mwamini Yesu ili atakapokuja akukute upo tayari, na ukaurithi uzima wa milele.

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/