Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Mtu anaposikia kiu anatafuta maji ya kunywa. Akinywa hayo maji, yanakuwa sehemu ya mwili wake. Hapo ndipo anapokuwa na afya njema kwa kunywa maji hayo. Mtunzi wa zaburi hii ana hamu kubwa ya kumwona Mungu. Hata amelinganisha hamu yake na kiu ya mnyama wa porini katika nchi ya ukame. Maadui za huyu Mwimba zaburi wanajaribu kumkatisha tamaa, lakini yeye anaamini Mungu atamhifadhi na kumsaidia. Tafakari ushuhuda katika m.8 na 11:Mchana Bwana ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, ... Nafsi yangu, kwa nini kuinama, na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; kwa maana nitakuja kumsifu Aliye afya ya uso wangu, na Mungu wangu. Ni heri kila mmoja wetu awe na kiu ya namna hii.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/