Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Hapo ndipo BWANA alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake akawahurumia watu wake.Pigo la nzige, ujumbe wa nabii na mateso waliyopata yamefanya wanyenyekee mbele za Mungu. Kwa watu wake wanaofanya hivyo, Mungu anakomesha mateso na kurejesha uponyaji kwa upendo na huruma zake. Pia anawarejeshea baraka walizokuwa wamezipoteza. Ukombozi huu unawapeleka katika maisha mapya ya kiroho na kumwabudu Mungu.Agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena(Yer 31:33-34). Imetupasa tuitike kwa Kristo Yesu kama tendo la ibada ya kweli kwa ajili ya alivyotuokoa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/