Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Musa anaagizwa kutengeneza madhabahu kwa ajili ya kufukizia uvumba. Isitumike kwa kutoa sadaka, bali iwe mfano wa sala na maombi yanayotolewa kwa Mungu katika heshima kubwa. Kuhusu sensa, pamoja na kila Mwisraeli kuhesabiwa, alipaswa kutoa sadaka maalumu. Hiyo ilikuwa ndogo hata mtu maskini aweze kulipa. Kwamba wote walipa sawa huleta usawa miongoni mwa watu wote wa taifa la Mungu. Huonyesha kuwa mbele yake tajiri hapendelewi kuliko maskini. Mungu hana ubaguzi, balitajiri na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye aliyewaumba wote wawili(Mit 22:2).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/