Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Haikuwa Musa tu aliyeitwa kumtumikia Mungu katika kuwaongoza Waisraeli. Kuna watu wengine waliopewa Roho wa Mungu ili kusaidiana naye kulingana na wajibu wa kila mmoja. Kuna wajenzi, masonara, washonaji n.k. kwa kadiri ya Mungu kuwaita. Kazi ya Mungu inafanywa na kila anayemwamini. Si wajibu wa mtu ama kundi fulani pekee. Amri ya Sabato ni nyeti kwa uhusiano kati ya Mungu na watu wake. Mungu anawakumbusha kuwa yeye ndiye anayewatakasa, na njia yake mojawapo ni hao kuishika Sabato, kama Mungu anavyokaza katika m.13:Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/