Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Mungu ameitenga siku moja kwa ajili ya kupumzika na kuabudu. Kwa Wayahudi ilikuwa ni Jumamosi. Kwetu Wakristo imekuwa ni Jumapili tangu wakati wa mitume. Walichagua siku hii iwe sabato yao kwa sababu Jumapili ni siku ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu. Kusudi la Mungu kutupa sheria hii ni kutulinda na kututendea mema. Kwa hiyo Yesu alisali kwa uaminifu siku hiyo,akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake(Lk 4:16). Alitumia pia siku hiyo kwa ajili ya kuwatendea mema walio karibu naye na walio na mahitaji. Katika m.1 imeandikwa kwambawanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.Mafarisayo walipomwambia Yesu kwamba wanafunzi wake walifanya lisilo halali, alijibu:Kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. Na katika m13-15 tunasoma jinsi Yesu alivyomwambia yule mtu mwenye mkono umepooza,Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, ukawa mzima kama wa pili. Tusiwe kama Mafarisayo waliompinga Yesu, bali tumfuate!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/