Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

SIKU 3 YA 31

Yesu anafundisha juu ya jambo moja ambalo kwa kawaida hukosekana kwa sisi wanadamu, yaaniunyenyekevu wa moyo mbele ya Mungu. Bila unyenyekevu huu hatuwezi kumtambua Mungu wala Mwana wake, Yesu Kristo. Yesu hujiweka mwenyewe kuwa mfano kwetu katika hili. Katika m.29 anasema:Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Ni jambo hili Paulo anakumbusha katika Flp 2:5-8, akiandika:Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye ... alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.Watoto wachanga pia ni mfano, maana wanahitaji kupokea kila kitu na wala hawawezi kuijisifia uwezo wowote. Katika m.25 Yesu anamwambia Mungu:Mambo hayauliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Basi, sikia wito wa Yesu katika m.28:Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha;ukajinyenyekeze mbele yake! Hivyoutapata raha nafsini mwako(m.29).

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/