Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

SIKU 2 YA 31

Tuliomboleza, wala hamkulia(m.17b). Hao ambao waliomboleza ni Yohana na wanafunzi wake. Walitumia sana kufunga. Kwa hiyo, badala ya kulia pamoja nao, watu walidai Yohana ana pepo.Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza(m.71a).Hao ambao walipiga filimbi ni Yesu na wanafunzi wake, maana kukaribia kwa ufalme wa Mungu ni neema kubwa, ni furaha ya ajabu. Katika Mit 8:12-36 kuna unabii juu ya Yesu Kristo (ukiwa na nafasi, tafuta kusoma kifungu hiki). Katika unabii huu Kristo anajitambulisha kwa kujiita "Hekima". Ndivyo Yesu anavyofanya hapa katika m.19b:Hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.Yaani, kazi yake Yesu inamshuhudia yeye ni nani. Hata hivyo wengi hawakutubu. Badala kucheza, Yesu alipowaletea habari hiyo njema kwamba ufalme wa Mungu umekaribia, walisema Yesu ni mlafi na mlevi. Katika m.20-24 Yesu anataja mifano ya watu hao, na kubainisha matokeo ya kumkataa.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana