Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Watanzania wengi wametolewa mapepo kwa jina la Yesu. Kwa hiyo tunahitaji kuwa makini sana kuyaangalia mafundisho ya Yesu katika m.43-45:Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya! Hapa Yesu anatuonyesha umuhimu wa kumtunza kiroho mtu wa namna hiyo. Huduma yetu haina maana, ikiwa mtu amesaidiwa kwa siku moja, wiki moja au mwaka mmoja tu. Asiposaidiwa kiasi cha kuweza kusimama imara katika Yesu na kufika Mbinguni, hatujafanikiwa huduma yetu. Kuna utupu katika moyo wa mtu baada ya kutolewa pepo. Ni lazima utupu huu ujazwe na neno la Mungu na sala!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/