Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

SIKU 6 YA 31

Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake(m.34). Neno hili linaonesha Yesu anavyoweka umuhimu sana kwa maneno yetu, maana tusemayo hufunua hali ya mioyo yetu. Paulo anakaza jambo hilohilo katika Rum 10:9-10:Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Mafarisayo walinena maneno mabaya juu ya Yesu. Walidai kwamba hutoa pepo kwa nguvu ya Shetani. Hayo maneno yao yanaonyesha kwamba ndani ya mioyo yao ni wabaya, kama tulivyoona katika m.34. Kipimo kingine cha hali ya mioyo yetu kinasomeka katika m.30 anaposema Yesu:Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. Huwezi kusimama katikati. Ama uko pamoja na Yesu au uko kinyume! Je, wewe unakusanya pamoja naye, yaani unawapenda walio wake na kuwavuta wengine kwake?

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/