Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 14 YA 31

Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema(m.8b). Haya ni maneno ya mtu ambaye ameshuhudia na ana uhakika na analolisema. Daudi alipita katika majaribu mengi na hatari nyingi, kama zile za kutoka Mfalme Sauli na hata maadui wa taifa la Wafilisti. Ushindi huo wote anaona ameupata kwa sababu ya wema wake Mungu tu, na si vinginevyo. Anatoa mwaliko kwa wengine kumtegemea Mungu. Hasa wanyenyekevu na maskini (m.2, 6) waliadhimishe jina la Bwana, kwani huwapa nuru wala hawatakosa kilicho chema.Wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema(m.10).

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha