Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano
Nami nitawafundisha kumcha BWANA(m.11b). Daudi anavaa ualimu wa hekima. Anamalizia zaburi hii kwa kukaza kuwa mtu akitaka uzima, basi aseme kweli, kufanya mambo mema na kutafuta amani kwa bidii. Ujumbe huohuo unapatikana katikaEbr 12:14,Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. Mungu anajibu maombi ya wanaoishi katika imani. Shida na matatizo visiwafanye watu kukaa mbali na Mungu, kwani Mungu siku zote anaweza kutuhifadhi na kutusaidia katika mambo hayo. Daudi anamalizia kwa kushuhudia kuwa hakuna hukumu ya adhabu juu yao wanaoishi hivyo na Mungu. Ndivyo anavyoshuhudia pia Paulo akisema,Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu(Rum 8:1).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/