Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 20 YA 31

Mungu aliwaonyesha watu wake wema maradufu. Kwanza aliwakomboa na mtesi, yaani mfalme wa Misri. Katika m.42 tunakumbushwasiku ile alipowakomboa na mtesi. Ndipo kwa miaka 40 Mungu akawaongoza watu wake safarini jangwani, akawakalisha katika nchi nzuri aliyowaahidia, akiwafukuza kwa nguvu watu wa mataifa mengine waliokaa humo(m.55, Aliwakalisha kabila za Israeli katika hema zao). Lakini Waisraeli walisahau wema huo. Hata walimwasi Mungu mara nyingi sana. Tumia sasa muda kidogo kuzingatia wema aliokuonyesha Mungu katika maisha yako, na linganisha na ulivyomtendea kwa sababu ya wema huo!

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/