Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano
Uasi wa Israeli ulikuwa ni pamoja na kunung’unika walipokuwa wahitaji. Hata hivyo Mungu aliwapa chakula cha kutosha wakiwa katika kosa hilo la kumjaribu. Lakini kwa kuwa Waisraeli hawakutubu wala hawakuwa na imani naye, Mungu akawaua. Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu. Hatutendei kwa ukali siku zote. Ana huruma hata tukingali wakosaji. Lakini ujumbe huu wa faraja ni kweli kwao tu walio wenye toba na wanyenyekevu. Ndivyo anavyoshuhudia Isaya katika Isa 57:15-16 akisema,Yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu. Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya. Kwa hiyo tuwe na toba, tumche, ili tuepuke hasira yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/