Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 16 YA 31

Mungu alichagua taifa la Israeli akiwaonyesha uweza wake kwa matendo makuu na kuwafundisha sheria zake ili wazitii. Lakini mara nyingi hawakumtii wala hawakuyakumbuka matendo yake ya uweza.Ili kizazi kingine wawe na habari(m.6), zaburi hii inafundisha maana ya kiroho ya matukio makuu katika historia ya Israeli. Lengo ni kwambawamwekee Mungu tumaini lao. Wala wasiyasahau matendo ya Mungu, Bali wazishike amri zake. Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu(m.7-8). Zingatia matokeo ya kupokea mafundisho ya namna hii! Hutusaidia kuweka tumaini kwa Mungu pekee, kukumbuka alivyotenda makuu, kumtii na kuepuka kuwa wakaidi na waasi.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha