Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 20 YA 31

Wasamaria walivutwa kumkaribisha Yesu mjini kwao kutokana na ushuhuda wa yule mwanamke Msamaria aliyekutana na Yesu kisimani. Nao walipomsikiliza Yesu wakamwamini na kushuhudia kuwa hakika Yesu ni Mwokozi wa ulimwengu (m.39-41, Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. ... Yesu akakaa huko siku mbili. Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake). Je, wewe pia unamwamini Bwana Yesu? Basi mshuhudie kwa neno na tendo. Pengine unafikiri utaanza baadaye, baada ya kujua zaidi jinsi ya kufanya? Basi, zingatia maana ya m.35, Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno (m.35). Ni sasa Yesu yupo tayari kukutumia kuleta wokovu kwa wengine.

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha