Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano
Yaliyoandikwa katika m.9 na 12 yanaonyesha kwamba mwanzoni yule mwanamke Msamaria alifikiri Yesu yu Myahudi wa kawaida tu: Yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? ... Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? Hatua ya pili mwanamke Msamaria alifikiri Yesu yu nabii anayeweza kumwongoza katika mambo kawaida ya kidini. Ndiyo maana akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia (m.19-20). Hatimaye alimtambua Yesu kuwa ndiye Masihi. Hapo yule mwanamke Msamaria akasahau kabisa kiu yake ya kimwili, maana alikuwa amepata maji ya uzima kutoka kwa Yesu na kutaka tu kumshuhudia yeye. Kwa hiyo akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo (m.28-29)? Nawe unaweza kumshuhudia Yesu vivyo hivyo kuwa ndiye mwokozi wako aliyekusaidia na kiu yako ya kiroho?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/