Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano
Malaki alifanya kazi kipindi cha Nehemia. Wakati huu Waisraeli wachache walirudi Yerusalemu toka Babeli. Hawakupata mafanikio, bali waliona ugumu wa maisha na umasikini. Hapo ndipo walipomlalamikia Mungu kuwa hawapendi. Mungu anawahakikishia kuwa bado anawapenda. Jinsi alivyomteua Yakobo kuwa wake na kumwacha Esau ni uthibitisho wa kutosha! Lakini pamoja na kutopenda, Mungu anachukia uovu. Hivyo wenye dhambi wasipotubu, hawatafanikiwa kama Edomu walivyoshindwa kufanikiwa. Edomu asema, Tumepondwa-pondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa. Lakini Bwana wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha ... (m.4).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/