Maelezo ya mpango
Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano
![Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F34662%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Jambo muhimu sana ni kiu ya kutafuta kuuingia ufalme wa Mungu. Nikodemo alikuwa nayo. Na wewe, je? Kama unayo kiu hii, basi, sikiliza kwa makini maelezo ya Yesu mwenyewe akifunua siri ya namna ya kuuingia ufalme wa Mungu: Zaliwa mara ya pili! Fikiria mtoto anavyozaliwa. Si utashi na nguvu zake mwenyewe zinazofanya hiyo, bali ni kazi ya mzazi. Kwa hiyo kuzaliwa mara ya pili ni tendo la Mungu. Mungu anamzaa mara ya pili kila mtu anayemwamini Yesu Kristo na kubatizwa kwa maji na kwa Roho.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F34662%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/