Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano
Leo tunaona ushuhuda zaidi wa Yohana Mbatizaji kumhusu Yesu na kwamba kazi yake haipingani na kazi ya Yesu. Kwa unyenyekevu Yohana anajilinganisha na mpambe wa bwana arusi, wakati Yesu ni bwana arusi: Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua (m.29-30). Tuutafakari unyenyekevu wa Yohana Mbatizaji tukirudia kusoma m.31-36: Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake. Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli. Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo. Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake. Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. Ukikumbuka maneno hayo, jipatie majibu mazuri kwa haya maswali muhimu sana: Je, Yesu alitoka wapi? Ana uhusiano gani na vyote? Na huu uhusiano una umuhimu gani kwa wamwaminio na wasiomwamini? Tumia muda kutafakari zaidi m.36 unaosema, Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/