Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 14 YA 31

Hekalu lilikuwa ni nyumba ya Mungu. Lilijengwa kwa matumizi ya sala, lakini Wayahudi waliligeuza kuwa mahali pa kufanyia biashara na dhuluma. Pamoja na kutakasa jengo lile, Yesu anawaonyesha Wayahudi kuwa hekalu la kweli ni mwili wake mwenyewe, na kutabiri kuhusu atakavyofufuka. Siku hizi Wakristo ni mwili wa Kristo. Hivyo miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yetu. Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu (1 Kor 3:16)? Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu (1 Kor 6:19)? Tukumbuke kuwa bado Yesu anataka hekalu la Mungu libaki kuwa mahali patakatifu na kazi yake iwe ileile ya kuwa nyumba ya sala!

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha