BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 31: Binti Hekima Mwanzo hadi Mwisho
Katika sura ya 31 mtu wa pili ambaye si Mwisraeli anazungumza. Kama Agul, Lemuel ni mwana mwenye hekima, lakini tofauti na Agur, Lemuel pia ni mfalme. Hii ni "hekima" ya Lemuel (mstari wa 1).
Hatujui chochote kuhusu Lemuel kama vile ni wapi au ni lini alikuwa mfalme, lakini kama ambavyo sura ya 30 ilianza na wasifu mfupi wa Agur (30:1-9), wasifu wa Lemuel pia unaelezwa (31:1-9). Tunaelezwa kuwa hekima yake yote ilitoka kwa mamake, aliyemwonya kuhusu wanawake na mvinyo na akamfundisha kuhusu kuwatetea maskini na wasiojiweza.
Wanawake ni wa muhimu sana kote katika Mithali kama tulivyoona hekima ikichukuliwa kuwa mwanamke (Sura ya 1-9) Shairi hili la mwisho linaendeleza maudhui haya kwa kuzungumzia kuhusu mwanamke fulani mwenye busara na anayedhihirisha busara ya kweli.
Shairi hili la mistari 22 limeundwa kama shairi jingine la kialfabeti la Kiebrania. Kila mstari unaanza kwa herufi mpya na unaonyesha jinsi mwanamke huyu ana hekima kutoka mwanzo hado mwisho. Anabariki nyumba yake na anasifiwa na familia yake. Kama tulivyomwona Binti Hekima mwanzoni mwa Mithali, ni hitimisho linalofaa kumwona mwanamke huyu mwenye busara anayeibariki nyumba yake na kusifiwa na familia yake. Ni taswira ya kuhamasisha maisha ya kutafuta hekima na baraka za Mungu.
Je, hekima imekusaidia vipi maishani? Je, unahitaji kwenda sambasamba na Mungu katika mambo gani?
Tumefikia mwisho wa kitabu cha Mithali. Kitabu hiki chote kinahusu jinsi ya kuishi vyema katika ulimwengu mzuri wa Mungu. Soma kitabu hiki tena na tena unapojenga maisha kwenye msingi wa hekima ya Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili