BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 23: Nini cha Kutokufanya
Tunapoendelea kusoma Misemo Thelathini ya Wenye Busara, tunaona kuwa mingi ni mashairi mafupi yenye urefu tofauti. Hapa katika sura ya 23 tunapata misemo ifuatayo 12.
Mingi ya misemo hii 12 inahusu kujizuia. Angalia jinsi maneno “usi,” “usiruhusu,” “usiwe” yamerudiwa. Kwa mzazi yeyote, haya ni maneno yaliyozoeleka sana. Mara kwa mara wazazi huwakanya watoto kwa kuwa wanawapenda, ili kuwalinda dhidi ya mabaya yanayotokana na matendo yao. Mtu yeyote anayetaka kuishi maisha mazuri yenye ufanisi anapaswa kujua kile anachotakiwa kukwepa kufanya. Baada ya muda, utazoea kujiepusha na mambo haya "Usiyotakiwa Kufanya".
Pia tunajifundisha kuwa mtu mwenye busara hujiepusha na kusifiwa, kujaribu kujitajirisha, kuzungumza sana, kuingilia mambo ya wengine, kutelekeza watoto wao, kutamani vitu vya watu wachoyo, kuwa karibu na marafiki wavivu, kutowaheshimu wazazi na kulewa sana.
Angalia jinsi neno “moyo” lilivyorudiwa katika sura hii (mstari wa 12, 15, 17, 19, 26, na 33) na “jicho” (mstari wa 5, 26, 31, na 33). Hizi ndizo njia za kuifikia nafsi ya mtu. Misemo hii ni maonyo ya kulinda mawazo na hisia zako. Unaposoma misemo hii, mwombe Bwana akuwezeshe kudhibiti tamaa zako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili