BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 27: Watu ni Muhimu Zaidi
Waandishi wa Hezekia walipanga mkusanyiko huu katika sehemu mbili, kila moja ikiwa na muundo na ujumbe wa kipekee. Sehemu ya 1 ina mistari wa 1-22. Kila mistari miwili katika sehemu ya 1 inazungumzia jambo moja. Sehemu ya 2 ni shairi moja linaloanzia mstari wa 23-27.
Sehemu ya 1: mstari wa 1-22— Alfabeti ya kiebrania ina herufi 22 na wasomi wengi wanaamini kuwa sehemu hii imepangwa kimahususi kuwa na mistari 22. Kila mistari miwili imewekwa pamoja (1-2,3-4, 5-6, n.k.) na inazungumzia stadi mbalimbali za mahusiano. Yaani, mithali hii ni "Mwongozo wa uhusiano mwema." Ukipuuza hekima hii, mahusiano yako yatateseka. Fuata ushauri wake na utakuwa na urafiki wa kudumu.
Sehemu ya 2: mstari wa 23-27— Sehemu hii ina shairi moja ndefu kuhusu uongozi na imejaa taswira za ukulima. Kusudi lake ni kukuza kiongozi (tazama mstari wa 24), na cha msingi ni kuwa kuongoza kunahitaji umakinifu na kujitunza kila wakati. Fursa na uwezo wa mtu hubadilika kila wakati. Njia ya pekee ya kudumisha utulivu ni kupitia kuwajali unaowaongoza.
Pamoja, sehemu ya 1 na 2 zinawasilisha ujumbe wazi: watu ni wa muhimu zaidi kuliko vitu. Wekeza nguvu yako katika watu. Fanya juhudi zinazohitajika ili kukuza mahusiano mema. Ni nani anayehitaji muda wako leo? Je, unaweza vipi kuwapa watu kipaumbele zaidi ya majukumu? Muombe Bwana maarifa unapoanza siku yako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili