BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 29: Hekima ya Kujizuia
Hii ndiyo awamu ya mwisho ya misemo ya busara iliyokusanywa na watumishi wa Hezekia. Sura hii inaanza kwa somo kuhusu kufunzika—moja ya maadili makuu ya mtu mwenye busara. Mwenye hekima anapaswa kusikiliza na kukubali kurekebishwa (tazama mstari wa 1). Tazama jinsi misemo hii inavyokamilika. Tunaambiwa tumche Bwana kuliko mwanadamu yeyote kwa kuwa haki yote inatoka Kwake (mstari wa 25-26). Kufundishika na kumwamini Mungu: maadili haya ndiyo msingi wa yote katika sura hii.
Kati ya mithali za mwanzo na zile za mwisho, kuna msisitizo mkali kuhusu kujidhibiti. Kiongozi mwenye busara sharti ajiongoze ikiwa angependa kuwaongoza wengine. Sharti tuwaongoze walio chini yetu (hasa watoto); tunahitaji kufanya hivi ikiwa tungependa kufurahia tunda tamu la hekima (mstari wa 15 na 17). Zingatia maadili haya matatu: kufundishika, kujizuia na kumwamini Mungu. Je, ni lipi ambalo Bwana anakuomba uzingatie zaidi?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili