BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 26: Jinsi ya Kutokuwa Mpumbavu
Sura ya 26 inazungumzia watu watano wenye sifa mbaya:
•Mpumbavu (sura ya 1-12)
•Mtu Mvivu (mstari wa 13-16)
•Mmbea (mstari wa 17-19)
•Mnong'onezaji (mstari wa 20-22)
•Mwenye Chuki (mstari wa 23-28)
Sura hii imejaa ulinganisho (maneno "kama" au "kama tu" yametumika sana), unaowafananisha watu hawa na mambo mabaya sana ("kama mwehu kutupa mishale ya kifo," ajabu!). Angalia ulinganishaji unaotumia vitu vya asili (shorewanda, farasi, punda, simba n.k.). Kwa jumla, ni wazi kuwa: usiwe mmoja wa watu hawa!
Usiwe Mpumbavu. Hafikirii na ni zuzu. Hawezi kuaminika, wala kutegemewa. Yeye ni mzigo kwa wote wanaomtuma. Usiwe Mvivu. Hutambua matatizo lakini hafanyi chochote kuyasuluhisha. Huanza kazi ambazo hajui jinsi ya kuzikamilisha. Anajichukulia kuwa mwerevu lakini hatoki kitandani.
Usiwe Mmbea. Hudadisi lakini hapati chochote ila majanga. Husababisha ugomvi kisha unauita mzaha. Usiwe Mnong'onezaji. Huchochea ugomvi na kuendeleza chuki. Hujua kuchochea uhasama na anaichukulia kuwa jambo la kufurahisha. Usiwe Mwenye Chuki. Huwa na kisasi na bado hujifanya kuwa rafiki. Hutoa sifa zisizostahiki na kuonyesha furaha lakini udanganyifu wake utajulikana.
Unaposoma sura hii, tenga muda uombe kuhusu kila mhusika ukitafakari kuhusu yanayotokana na njia zao za maisha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili