BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 30: Mafumbo ya Mwenye Busara
Sura ya 30 na 31 ni hitimisho la kitabu hiki cha kale cha hekima kwenye biblia. Cha kushangaza, kila sura ina mashairi yanayohusishwa na waandishi wasio waisraeli waitwao Agur na Lemuel. Agur ni mtu wa kawaida, naye Lemuel ni mfalme. Kulingana na maelezo yaliwekwa, wote wanarejelewa kama wana— hitimisho hili ni mwafaka kwani kitabu hiki kinahusu wana kupata hekima.
Katika sura ya 30 tunasikia kutoka kwa mwana wa kwanza mwenye busara, Agur. Kuna wasifu mfupi katika mstari wa 1-9, ikifuatwa na mafumbo ya kuvutia (mstari wa 10-13). Mafumbo mengi kati ya haya yanazungumzia mambo ambayo unapaswa kujiepusha nayo: masengenyo, kulaani, chuki, udanganyifu, dhihaka, uzinzi, kiburi na uovu. Japo haya ni maovu, misemo ya Agur inaonyesha kuwa wanaofanya mambo haya hujichukulia kuwa wasio na hatia.
Baadhi ya mafumbo haya hayahusu maadili au tabia njema, bali yanazungumzia uhusiano na mambo ya kawaida. Mafumbo haya yana sehemu tatu. Sehemu mbili za kwanza zinazungumzia kuhusu jinsi ulimwengu ulivyo. Ya tatu inaonyesha jinsi sehemu ya kwanza na ya pili zinahusu namna hekima inavyofanya kazi.
"Kama vile malai huunda siagi (sehemu ya 1), na kama vile kuikunja pua huvujisha damu (sehemu ya 2), hivyo kuchochea hasira huleta ugomvi" (sehemu ya 3).
Mafumbo pamoja na wasifu yanatuchochea tufikirie matokeo ya uamuzi na matendo yetu. Je, unapaswa kuzingatia nini zaidi unapoianza siku yako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili