BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 28: Simba Mzuri, Simba Mbaya
Kama tunavyofahamu, sura ya 25-29 zilipangwa na watumishi wa Mfalme Hezekia takribani miaka 250 baada ya Mfalme Sulemani. Sehemu ya kwanza (sura ya 25-27) ni kwa watu wanaowatumikia viongozi, lakini sehemu hii ya pili (sura ya 28-29) inalenga viongozi.
Zaidi ya hayo, muundo wa kifasihi wa sehemu hii ni wa kuvutia! Ina mithali 28, huku 14 zikiwa katika nusu ya kwanza na 14 katika nusu ya pili. Kila sehemu inaanza kwa mithali kuhusu simba (mstari wa 1 na 15). Mmoja kati yao ni mzuri, mwingine ni mbaya. Mmoja ni jasiri na mwenye heshima na mwingine huhema tu na kunguruma. Simba, kwa kawaida, ni ishara ya uongozi. Utakuwa kiongozi wa aina gani? Anayetumia wadhifa wake kuwalinda wengine, au anayetumia mamlaka kujinufaisha?
Kulingana na sura hii, kiongozi mwenye busara na mwenye haki ana moyo wa huruma. Tazama ni mara ngapi maskini na waliokandamizwa wametajwa katika sura hii. Anayewajali wasiojiweza huonyesha heshima ya kweli, lakini amelaaniwa anayewapuuza maskini (mstari wa 27). Huenda usijione kama mtawala au kiongozi, lakini sote huongoza kwa kiwango fulani, hata kama ni miongoni mwa marafiki na familia. Hebu mithali hizi zikupe changamoto kuhusu jinsi unavyoishi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili