Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Hekima ya MithaliMfano

BibleProject | Hekima ya Mithali

SIKU 25 YA 32

Sura ya 24: Maneno Mazuri, Kazi Mbaya

Sehemu ya kwanza ya sura hii (1-22) ina misemo ya mwisho kumi na miwili kati ya Misemo Thelathini ya wenye Busara. Maudhui ya “usifanye” kwenye sura ya 23 yanaendelea hapa: usione wivu (1), usiseme uongo (15), na kadhalika (tazama mstari wa 17, 19, 21). Hekima hudhihirishwa kupitia kujidhibiti; tamaa hudhibitiwa na nidhamu.

Kwenye mstari wa 23, tunapata misemo michache mipya iitwayo "Misemo ya Ziada ya Wenye Busara" (mstari wa 23-34). Yafuatayo ni mafundisho makuu yanayotokana na misemo hii:

•Mstari wa 23b-25 Hukumu ya haki

•Mstari wa 26 Maneno mazuri

•Mstari wa 27 Kazi nzuri

•Mstari wa 28-29 Maneno mabaya

•Mstari wa 30-34 Kazi mbaya

Mstari wa 23b-25 unatufundisha kutambua mazuri na mabaya katika maneno na matendo. Hebu fikiria, maneno na matendo ndiyo maisha ya mtu kwa jumla na hubaini kiwango cha maisha. Je, ukitathmini maisha yako kulingana na misemo hii, hali ikoje?

Andiko

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili