Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Pauli aliona nimfungwa wa Kristo(m.1,Mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa). Ameitwa naye kwenye huduma kati ya watu wa mataifa. Kwa neema alifunuliwa siri kuhusu hao. Hakubuni mwenyewe. Anatumia neno “siri” mara tatu katika kifungu hiki (m.3, 4 na 5,Kwa kufunuliwa nalijulishwasiri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katikasiri yakeKristo.Siri hiyohawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho). Siri ni kweli fulani ambayo wanadamu hawakujua mpaka Mungu alipowafunulia. Ni siri kwa sababu awali wanadamu hawakuelewa watu wa mataifa watakubalika na Mungu sawa na Wayahudi. Kufa kwa Yesu kulifidia dhambi za watu wote, hivyo akawakomboa wote. Mbele ya Mungu sisi sote tu sawa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/