Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Njia ya kumkaribia Mungu ni moja tu (Yn 14:6,Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, ... mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi). Mpatanishi ni mmoja tu. Kristo alikuja akahubiri amani kwa wote (m.17,Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu). Kwa kupitia Kristo tunaweza kumkaribia Mungu Baba (m.18,Kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja). Kwa hiyo Myahudi ataokolewa kwa neema sawa na Mmataifa. Amani ni kwa wale waliokuwa mbali na kwa wale waliokuwa karibu. Wageni wamekuwa wenyeji, na wote ni wa familia moja. Wote ni wa jamii mpya ya wanadamu ambayo Mungu ameiunda kwa njia ya Kristo (m.19,Tangu sasa ... ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu). Je, umeshajiunga na jamii hiyo? Kwa tafakari zaidi juu sifa zake rudia m.20-21,Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/