Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Wakristo wa mataifa wanakumbushwa hali yao kabla ya Kristo (m.11-12,Kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili ... mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani). Walikuwa nje ya watu wa Mungu.Lakini sasahali yao imebadilika (m.13,Ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo). Badiliko ni kuwa na Kristo. Amewaleta karibu, kwa sababu ya upatanisho uliofanyika katika kifo chake. Halafu, baada ya kuwaleta karibu, aliwaunganisha na watu wake wa Kiyahudi. Hao wawili tofauti walifanywa kuwa mtu mmoja katika Kristo (m.14,Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga). Kwa hiyo Myahudi ataokolewa kwa neema sawa na Mmataifa (m.17-18,Kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja). Je, hali yako imebadilika vivyo hivyo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/