Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 6 YA 28

Waumini wameketi pamoja na Kristo katika ulimwengu wa mbinguni kutokana na wao kuungana naye (m.6,Akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu). Kristo mwenyewe ni haki yao ya kuwa na uenyeji huu wa mbinguni (Flp 3:20,Wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo). Wokovu ni kwa neema na kupokelewa kwa imani pekee (m.8,Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu). Imani inayookoa inahusisha ufahamu wa Injili, na kuamini habari yake ni ya kweli kwa kujikabidhi mikononi mwa Kristo. Wakati waumini wanaokolewa kwa imani, na wala siyo matendo mema, imani inayookoa kila wakati inadhihirishwa kwa matendo mema (m.10,Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo).

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/