Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Paulo alitaka wajue habari za kweli juu yake. Alikuwa kifungoni, na wengi walikuwa na wasiwasi kwa sababu ya dhiki yakeBasi naomba msikate tamaa kwa sababu ya dhiki zangu kwa ajili yenu, zilizo utukufu kwenu(3:13). Paulo alimtuma Tikiko. Kwa lugha ya upendo anamtaja kama “ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana” (m.21). Salamu zake za mwisho ni kama maombi:Amani na iwe kwa ndugu, na pendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo katika hali ya kutokuharibika(m.23-24). Ombi la mwisho linahusu neema ya Mungu, ambayo amerudia kutaja mara kwa mara katika waraka. “Wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo” ni mkazo kuwa neema hiyo inadumu kwao tu wanaoendelea kupendana na Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/