Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Kukombolewa na Yesu hufungamana na hekima ya Mungu (1:7-8,Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi). Ni hekima ya kiutendaji. Wenye hekima hiyo huanza “kuukomboa wakati” (m.16). Wameelewa kwamba nyakati zao ni za uovu, kwa hiyo waishi kwa hekima ya kuutumia wakati vizuri. Je, wewe ni mmoja wapo? Nini mahusiano yako na kileo? Mara nyingi ulevi unaandamana na maovu, maana watu wakiwa chini ya kileo wanashindwa kutawala matendo yao (m.18,Msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi). Tukikubali kujazwa na Roho, atatutawala. Matokeo yake ni matendo ya kumsifu Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/