Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 22 YA 28

Pia wajibu wa mume kwa mke hufungamana na hali hiyohiyo wanayoshirikiana wote wawili, yaanihali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo(m.21). Mume anatakiwa kumpenda mkewe kwa kujitoa kwa ajili yake kama Kristo kwa Kanisa (m.25-26,Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno). Nadhani mume ana wajibu mkubwa zaidi (kujitoa) kuliko mke (kutii). Katika Mwa 2:21-24 twaona jinsi mke ni sehemu ya mwili wa mumewe, maana kutoka ubavu wa mwanaume Mungu alimfanya mwanamke. Kwa hiyo katika kumtunza mkewe, mume hujitunza mwenyewe: ”Apendaye mkewe hujipenda mwenyewe” (m.29). Mume, ni matendo gani katika maisha yako yanayoonyesha unampenda mke wako?

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/