Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 26 YA 28

Wale wote ambao wamejitoa kwa Mungu, amewakomboa kutoka katika kufuata mapenzi ya shetani (2:1-2,Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi). Sasa wanaishi katika mapenzi ya Mungu. Hivyo wameingizwa katika vita iliyopo kati ya Kristo na shetani. Somo la leo latufundisha kuhusu adui wetu. Kushindana kwetu si juu ya wanadamu, bali ni juu ya falme na mamlaka ya giza, yaani juu ya enzi zile zisizoonekana zilizo katika ulimwengu wa roho (m.12,Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho). Enzi hizo zina nguvu, ni ovu, zinatoa giza na hazipendi nuru, na zinaongozwa na shetani.Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama(m.13).

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/