Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Ili uwepo uhusiano mwema katika familia, wajibu wa watoto kwa wazazi ni utii. Kwa kurudia 5:21 inayosema,“hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo”, imeongezwa kuwa utii huu ni “katika Bwana” (m.1). ”Hii ndiyo haki,” yaani inalingana na utaratibu wa uumbaji. Kuwaheshimu wazazi pia hufuatana na ahadi ya kuishi siku nyingi (Kut 20:12,Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako). Wazazi, tusiamrishe mambo yasiyo halali kwa watoto wala tusiwachokoze, bali tufuate miongozo ya Kikristo katika maisha yetu wenyewe na kwa kuwalea watoto wetu katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/