Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 25 YA 28

Neno kuhusu uhusiano mwema wa bwana na mtumwa pia lawahusu wafanyakazi na wakubwa wao. Watumwa wanatakiwa kuwatii walio bwana zao hapa duniani (m.5,Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili ... kana kwamba ni kumtii Kristo). Maana yake, wote wanaye Bwana aliye juu mbinguni, naye pia ni Bwana juu ya uhusiano wao. Wafanyakazi, tusifanye kazi kwa kujipendekeza, bali kwa kumtazama Bwana Yesu (m.6,wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo). Wajibu wa mabwana ni kuwatendea walio chini haki, kwani nao wanaye Bwana aliye mbinguni. Mtumwa na bwana, wote wawili wako sawa katika kuwa na Bwana mmoja asiye na upendeleo.

Andiko

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/