Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Silaha zina Mungu, ni juu yetu kuzivaa tu.Ukweli wa Injili: Utatulinda dhidi ya mafundisho ya uongo wa aina zote.Dirii ya haki kifuani: Mtu amwaminiye Kristo Yesu amevikwa haki yake.Kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya imani: Miguu iliyowekwa katika misingi imara ya Injili haitelezi, tena tunatiwa hamu ya kuishuhudia.Ngao ya imani:Imani katika Yesu inazuia mishale yote ya adui.Chepeo ya wokovu: Hiki ni kipawa cha Mungu.Upanga wa Roho: Neno la Mungu ni silaha ya kushambulia adui.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/