Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Kristo ni mwili na sisi tu viungo vya huo mwili. Huu ni ukaribu mkubwa kati ya Wakristo na Kristo. Mfano wake ni kama mke alivyo sehemu ya karibu na mumewe, na mume anavyompenda na kumtunza mkewe kana kwamba ni mwenyewe. Mfano mwingine ni ule wa mzabibu. Bwana wetu Yesu Kristo yu karibu sana hali ameungana nasi kama mti na matawi yake (Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote;soma mwenyewe mistari yote ya Yn 15:1-7). Hivyo ndivyo kusudi la ndoa: Mume mmoja na mke mmoja waishi pamoja kama watu wawili waliojiunga katika ndoa kuwa kama mwili mmoja (m.31,Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/